Tefsîru'l-Müyesser — Svahili tercümesi (tefsir) — Al-Layl 92:1 – Al-Nas 114:6
Contents
- Al-Layl 92:1
- Al-Layl 92:2
- Al-Layl 92:3
- Al-Layl 92:4
- Al-Layl 92:5
- Al-Layl 92:6
- Al-Layl 92:7
- Al-Layl 92:8
- Al-Layl 92:9
- Al-Layl 92:10
- Al-Layl 92:11
- Al-Layl 92:12
- Al-Layl 92:13
- Al-Layl 92:14
- Al-Layl 92:15
- Al-Layl 92:16
- Al-Layl 92:17
- Al-Layl 92:18
- Al-Layl 92:19
- Al-Layl 92:20
- Al-Layl 92:21
- Al-Duha 93:1
- Al-Duha 93:2
- Al-Duha 93:3
- Al-Duha 93:4
- Al-Duha 93:5
- Al-Duha 93:6
- Al-Duha 93:7
- Al-Duha 93:8
- Al-Duha 93:9
- Al-Duha 93:10
- Al-Duha 93:11
- Al-Sharh 94:1
- Al-Sharh 94:2
- Al-Sharh 94:3
- Al-Sharh 94:4
- Al-Sharh 94:5
- Al-Sharh 94:6
- Al-Sharh 94:7
- Al-Sharh 94:8
- Al-Tin 95:1
- Al-Tin 95:2
- Al-Tin 95:3
- Al-Tin 95:4
- Al-Tin 95:5
- Al-Tin 95:6
- Al-Tin 95:7
- Al-Tin 95:8
- Al-'Alaq 96:1
- Al-'Alaq 96:2
- Al-'Alaq 96:3
- Al-'Alaq 96:4
- Al-'Alaq 96:5
- Al-'Alaq 96:6
- Al-'Alaq 96:7
- Al-'Alaq 96:8
- Al-'Alaq 96:9
- Al-'Alaq 96:10
- Al-'Alaq 96:11
- Al-'Alaq 96:12
- Al-'Alaq 96:13
- Al-'Alaq 96:14
- Al-'Alaq 96:15
- Al-'Alaq 96:16
- Al-'Alaq 96:17
- Al-'Alaq 96:18
- Al-'Alaq 96:19
- Al-Qadr 97:1
- Al-Qadr 97:2
- Al-Qadr 97:3
- Al-Qadr 97:4
- Al-Qadr 97:5
- Al-Bayyinah 98:1
- Al-Bayyinah 98:2
- Al-Bayyinah 98:3
- Al-Bayyinah 98:4
- Al-Bayyinah 98:5
- Al-Bayyinah 98:6
- Al-Bayyinah 98:7
- Al-Bayyinah 98:8
- Al-Zalzalah 99:1
- Al-Zalzalah 99:2
- Al-Zalzalah 99:3
- Al-Zalzalah 99:4
- Al-Zalzalah 99:5
- Al-Zalzalah 99:6
- Al-Zalzalah 99:7
- Al-Zalzalah 99:8
- Al-'Adiyat 100:1
- Al-'Adiyat 100:2
- Al-'Adiyat 100:3
- Al-'Adiyat 100:4
- Al-'Adiyat 100:5
- Al-'Adiyat 100:6
- Al-'Adiyat 100:7
- Al-'Adiyat 100:8
- Al-'Adiyat 100:9
- Al-'Adiyat 100:10
- Al-'Adiyat 100:11
- Al-Qari'ah 101:1
- Al-Qari'ah 101:2
- Al-Qari'ah 101:3
- Al-Qari'ah 101:4
- Al-Qari'ah 101:5
- Al-Qari'ah 101:6
- Al-Qari'ah 101:7
- Al-Qari'ah 101:8
- Al-Qari'ah 101:9
- Al-Qari'ah 101:10
- Al-Qari'ah 101:11
- Al-Takathur 102:1
- Al-Takathur 102:2
- Al-Takathur 102:3
- Al-Takathur 102:4
- Al-Takathur 102:5
- Al-Takathur 102:6
- Al-Takathur 102:7
- Al-Takathur 102:8
- Al-'Asr 103:1
- Al-'Asr 103:2
- Al-'Asr 103:3
- Al-Humazah 104:1
- Al-Humazah 104:2
- Al-Humazah 104:3
- Al-Humazah 104:4
- Al-Humazah 104:5
- Al-Humazah 104:6
- Al-Humazah 104:7
- Al-Humazah 104:8
- Al-Humazah 104:9
- Al-Fil 105:1
- Al-Fil 105:2
- Al-Fil 105:3
- Al-Fil 105:4
- Al-Fil 105:5
- Quraysh 106:1
- Quraysh 106:2
- Quraysh 106:3
- Quraysh 106:4
- Al-Ma'un 107:1
- Al-Ma'un 107:2
- Al-Ma'un 107:3
- Al-Ma'un 107:4
- Al-Ma'un 107:5
- Al-Ma'un 107:6
- Al-Ma'un 107:7
- Al-Kawthar 108:1
- Al-Kawthar 108:2
- Al-Kawthar 108:3
- Al-Kafirun 109:1
- Al-Kafirun 109:2
- Al-Kafirun 109:3
- Al-Kafirun 109:4
- Al-Kafirun 109:5
- Al-Kafirun 109:6
- Al-Nasr 110:1
- Al-Nasr 110:2
- Al-Nasr 110:3
- Al-Masad 111:1
- Al-Masad 111:2
- Al-Masad 111:3
- Al-Masad 111:4
- Al-Masad 111:5
- Al-Ikhlas 112:1
- Al-Ikhlas 112:2
- Al-Ikhlas 112:3
- Al-Ikhlas 112:4
- Al-Falaq 113:1
- Al-Falaq 113:2
- Al-Falaq 113:3
- Al-Falaq 113:4
- Al-Falaq 113:5
- Al-Nas 114:1
- Al-Nas 114:2
- Al-Nas 114:3
- Al-Nas 114:4
- Al-Nas 114:5
- Al-Nas 114:6
Al-Layl 92:1
Allah Mtukufu Anaapa kwa usiku unapoifunika ardhi na vilivyoko juu yake kwa giza lake.
Al-Layl 92:2
Na kwa mchana unapochomoza mwangaza wake kutoka kwenye giza la usiku.
Al-Layl 92:3
Na kwa kuumba aina mbili: ya kiume na ya kike.
Al-Layl 92:4
Kuwa hakika vitendo vyenu vinatofautiana: kuna wanaofanya kwa ajili ya dunia na wanaofanya kwa ajili ya akhera.
Al-Layl 92:5
Ama mwenye kutoa kwenye mali yake, akamcha Allah Mtukufu katika huko kutoa.
Al-Layl 92:6
Na akaamini «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na Imani hiyo, na akaamini malipo yanayofungamana nayo.
Al-Layl 92:7
Basi huyo tutamuongoza na kumuafikisha kwenye njia za kheri na wema na kumsahilishia mambo yake.
Al-Layl 92:8
Na ama mwenye kuifanyia ubakhili mali yake, akawa hana haja na malipo ya Mola wake.
Al-Layl 92:9
Na akakanusha neno la «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na neno hilo na akakanusha malipo yanayofungamana nalo.
Al-Layl 92:10
Tutamnyoshea njia za mateso.
Al-Layl 92:11
Wala haitamfaa kitu mali yake aliyoifanyia ubakhili atakapotumbukia Motoni.
Al-Layl 92:12
Ni juu Yetu, kwa fadhila Zetu na busara zetu, kueleza njia ya uongofu yenye kufikisha kwa Allah Mtukufu.
Al-Layl 92:13
Na Sisi Tuna mamlaka ya maisha ya Akhera na maisha ya ulimwenguni.
Al-Layl 92:14
Ndipo nikawaonya, (enyi watu), na moto wenye kuwaka, nao ni moto wa Jahanamu.
Al-Layl 92:15
Hataingia Moto huo isipokuwa aliyekuwa muovu zaidi, Mwenye kumkanusha Nabii Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).
Al-Layl 92:16
Ambaye amekataa kumuamini na kumtii Allah Mtukufu na Mtume wake.
Al-Layl 92:17
Na ataepushwa na moto huo mchaji Allah Mtukufu kwa wingi.
Al-Layl 92:18
Ambaye hutoa mali yake kwa kutaka nyongeza za kheri.
Al-Layl 92:19
Kutoa Kwake si kwa kulipa wema aliofanyiwa na mtu.
Al-Layl 92:20
Lakini anatoa kwa kutaka uso wa Mola wake na radhi zake.
Al-Layl 92:21
Basi Allah Mtukufu atampa huko peponi malipo ya kumridhisha.
Al-Duha 93:1
Allah Mtukufu Anaapa kwa wakati wa dhuha, na uliokusudiwa ni wakati wa mchana mzima.
Al-Duha 93:2
Na kwa usiku utuliapo na viumbe na likakolea giza lake. «Allah Mtukufu Huapa kwa Atakacho katika viumbe vyake. Ama kiumbe, hafai kuapa kwa asiyekuwa Muumba wake, Kuapa kwa asiyekuwa Allah Mtukufu ni ushirikina».
Al-Duha 93:3
Hakukuwacha Mola wako, (ewe Mtume), wala Hakukuchukia kwa kuchelewesha kukuteremshiaWahyi.
Al-Duha 93:4
Na Nyumba ya Akhera ni bora kwako kuliko nyumba ya ulimwengu.
Al-Duha 93:5
Na Atakupa Mola wako, (ewe Mtume), neema ya kila sampuli uridhike.
Al-Duha 93:6
Kwani hakukukuta, kabla ya hapo, ukiwa ni yatima, akakuhifadhi na kukutunza?
Al-Duha 93:7
Na akakukuta hujui chochote kuhusu kitabu wala Imani, Akakufundisha yale amabayo ulikuwa huyajui na akakupa taufiki ya kufanya matendo mema?
Al-Duha 93:8
Na akakukuta masikini, Akakuletea riziki yako, na Akakutajirisha kwa kutosheka na kusubiri?
Al-Duha 93:9
Basi yatima usimtendee ubaya.
Al-Duha 93:10
Na muombaji usimkaripie, bali mlishe na umtimizie haja zake.
Al-Duha 93:11
Na neema alizokupa mola wako zielezee.
Al-Sharh 94:1
Kwani Hatukukunjulia, (ewe Mtume), kifua chako kwa sheria za Dini, kulingania watu kwa Allah Mtukufu, na kujipamba kwa tabia nzuri?
Al-Sharh 94:2
Na tukakuondolea mazito yako?
Al-Sharh 94:3
Mazito yaliyolemea mgongo wako?
Al-Sharh 94:4
Na Tukakunyanyua, kwa matukufu Tuliyokuneemesha kwenye cheo cha juu?
Al-Sharh 94:5
Usirudi nyuma katika kueneza ujumbe uliotumwa nao kwa maudhi ya maadui zako. Kwani kwenye uzito kuna wepesi.
Al-Sharh 94:6
Hakika kwenye uzito kuna wepesi.
Al-Sharh 94:7
Basi utakapomaliza mambo ya kidunia na shughuli zake jipinde kwa kufanya ibada.
Al-Sharh 94:8
Na kwa Mola wako Peke Yake weka matumaini yako.
Al-Tin 95:1
Allah Mtukufu Anaapa kwa tini na zaituni, nayo ni miongoni mwa matunda yanayojulikana.
Al-Tin 95:2
Na Anaapa kwa jabali la Ṭūr Sīnā’ «ambalo Allah Mtukufu Alisema na Mûsã juu yake».
Al-Tin 95:3
Na Anaapa kwa Mji huu wa amani, «usiokuwa na mambo ya kutisha, Nao ni mji wa Makkah, chimbuko la Uislamu».
Al-Tin 95:4
Hakika Tumemuumba binadamu katika sura nzuri.
Al-Tin 95:5
Kisha Tutampeleka Motoni akiwa hatamtii Allah Mtukufu na kuwafuata Mitume.
Al-Tin 95:6
Isipokuwa wale walioamini na wakafanya amali njema; wao watakuwa na malipo makubwa yasiyokatika wala kupungua.
Al-Tin 95:7
Ni lipi linalokupelekea (ewe binadamu), kukanusha kufufuliwa na kulipwa, hali ya kuwa kuna dalili za wazi kwamba Allah Mtukufu Ana uwezo wa kufanya hayo?
Al-Tin 95:8
Je, Hakuwa Allah Mtukufu, Ambaye Ameiweka Siku hii kutoa uamuzi baina ya watu, ni muadilifu zaidi ya wanaosifika kuwa ni waadilifu katika kila Alichokiumba? kwani walidhani wataachwa Hivihivi tu: hawaamrishwi wala hawakatazwi wala hawalipwi kwa mema wala hawateswi kwa mabaya? Hilo si sahihi wala haliwi.
Al-'Alaq 96:1
Soma, ewe Nabii, Qur’ani uliyoteremshiwa ukianza kwa Jina la Mola wako Aliyepwekeka kwa kuumba.
Al-'Alaq 96:2
Aliyemuumba kila binadamu kwa pande la damu nzito nyekundu.
Al-'Alaq 96:3
Soma, (ewe Nabii), kile ulichoteremshiwa, na Mola wako ni Mwingi wa wema, Mwingi wa ukarimu.
Al-'Alaq 96:4
Aliyewafundisha viumbe vyake kuandika kwa kalamu.
Al-'Alaq 96:5
Alimfundisha binadamu vitu ambavyo hakuwa akivijua. Akamtoa kwenye giza la ujinga, Akampeleka kwenye nuru ya elimu.
Al-'Alaq 96:6
Kweli, binadamu hukiuka mipaka ya Allah Mtukufu
Al-'Alaq 96:7
Akijiona ametosheka kwa utajiri wake.
Al-'Alaq 96:8
Basi, ajue kila mwenye kuchupa mipaka kuwa uhakika ni kuwa atarudi kwa Allah Mtukufu Ambaye Atamlipa kila binadamu kwa alilolitenda.
Al-'Alaq 96:9
Je, umeona ujeuri wa ajabu zaidi kuliko wa mtu huyu, (Abû jahl), Anayemkataza mja wetu? «Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie»,
Al-'Alaq 96:10
Unamuona anavyomkataza mja wetu pale anaposwali?
Al-'Alaq 96:11
Waonaje iwapo mwenye kukatazwa kuswali yuko kwenye uongofu, vipi anamkataza?
Al-'Alaq 96:12
Au iwapo anaamrisha mwingine kumcha Mungu, vipi anamkataza hilo?
Al-'Alaq 96:13
Waonaje iwapo huyu mwenye kukataza anakanusha lile alinganiwalo kwalo na kulipa mgongo?
Al-'Alaq 96:14
Hajui kuwa Allah Mtukufu anaona kila analolifanya?
Al-'Alaq 96:15
Basi mambo si kama anvyodai Abū Jahl. Na asipokomeka na ushindani alionao na udhia wake, Tutamshika paji lake kwa nguvu na kumtia Motoni.
Al-'Alaq 96:16
Paji lake ni paji lenye maneno ya urongo na vitendo vya makosa.
Al-'Alaq 96:17
Basi na awalete, mchupaji mipaka huyu, watu wa baraza ili wamsaidie.
Al-'Alaq 96:18
Sisi Tutawaita Malaika wa adhabu.
Al-'Alaq 96:19
Mambo si kama Abû Jahl anavyoyadhania. Yeye, (ewe Mtume), hawezi kukufanya lolote la kukudhuru, Usimfuate kwa lile alilokuitia la kuwa uache Swala, bali msujudie Mola wako na uwe karibu naye kwa kujipendekeza Kwake kwa kumtii.
Al-Qadr 97:1
Sisi Tumeiteremsha Qur’ani katika usiku wa cheo na utukufu, nao ni miongoni mwa masiku ya mwezi wa Ramdhani.
Al-Qadr 97:2
Na nilipi liliokujulisha, (ewe Mtume), ni upi usiku wa cheo na utukufu?
Al-Qadr 97:3
Usiku wa cheo na utukufu ni bora fadhila zake kuliko fadhila za miezi elfu moja isiyokuwa usiku huo.
Al-Qadr 97:4
Usiku huo hushuka Malaika na Jibrili, amani iwashukie, kwa ruhusa ya Mola wao na kila amri ya kila jambo Alilolikadiria liwe kwa mwaka mzima.
Al-Qadr 97:5
Usiku huo wote ni amani, hakuna shari, mpaka kuchomoza alfajiri.
Al-Bayyinah 98:1
Haikua kwa wenye kukufuru miongoni mwa mayahudi na manaswara na washirikina ni wenye kuacha ukafiri wao isipokua mpaka iwajie alama walioahidiwa katika vitabu vilivyopita, yani walikua wanadai kua wakiona hiyo alama wataamini, lakini wakageuka isipokua wachache.
Al-Bayyinah 98:2
Na alama hiyo ni Mtume wa Allah Mtukufu, Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), mwenye kuwasomea Qur’ani iliyomo kwenye kurasa zilizo safi.
Al-Bayyinah 98:3
Ndani ya kurasa hizo mna habari za kweli na amri za uadilifu zenye kuongoza kwenye haki na kwenye njia iliyonyooka.
Al-Bayyinah 98:4
Na hawakutofautiana wale waliopewa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na manaswara, juu ya kuwa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ni Mtume wa kweli, kwa sifa zake walizokua wakiziona katika vitabu vyao, isipokuwa baada ya kuwathibitikia kuwa yeye ndiye Nabii waliyeahidiwa katika Taurati na Injili. Walikuwa wanakubali, kwa umoja wao, kuwa unabii wake ni wa kweli. Lakini alipopewa utume walimkanusha na wakatofautiana.
Al-Bayyinah 98:5
Na hawakuamrishwa katika sheria zote zilizopita isipokuwa wameamrishwa wamuabudu Allah Mtukufu Peke Yake, wakikusudia kwa ibada zao kupata Radhi Zake, na kuepuka ushirikina na kuelekea kwenye Imani, wasimamishe Swala na watoe Zaka. Kufanya hayo ndio Dini iliyonyooka, nayo ni Uislamu.
Al-Bayyinah 98:6
Hakika wale waliokufuru miongoni mwa Mayahudi na manaswara na Washirikina, mateso yao ni Moto wa Jahanamu. Watakuwa ni wenye kukaa milele humo, Wao ndio viumbe waovu kabisa.
Al-Bayyinah 98:7
Hakika wale waliomuamini Allah Mtukufu, wakamfuata Mtume wake na wakafanya amali njema, wao ndio viumbe bora.
Al-Bayyinah 98:8
Malipo yao, mbele ya Mola wao Siku ya Kiyama, ni Pepo ya makazi na utulivu, yenye upeo wa uzuri, ambayo chini ya majumba yake ya fahari inapita mito; watakaa milele humo. Allah Mtukufu Ameridhika nao, Akakubali amali zao njema. Na wao wameridhika naye kwa mapokezi Aliyowafanyia ya aina mbalimbali za takrima. Malipo mazuri hayo ni ya aliyemuogopa Mweyezi Mungu na akajiepusha na maasi.
Al-Zalzalah 99:1
Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu.
Al-Zalzalah 99:2
Na ikatoa vilivyomo ndani yake: miongoni mwa wafu na thamani za ardhini kama dhahabu na mfano wake.
Al-Zalzalah 99:3
Na akauliza binadamu, katika hali ya kubabaika, «imepatwa na nini?»
Al-Zalzalah 99:4
Siku hiyo (siku ya kiama) ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubaya.
Al-Zalzalah 99:5
Kwa kuwa Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, ataiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa.
Al-Zalzalah 99:6
Siku hiyo watu wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu kwa makundi, ili Allah Mtukufu Awaoneshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo.
Al-Zalzalah 99:7
Yoyote mwenye kufanya jema hata kama ni kwa uzito wa Mdudu Chungu atayaona malipo yake Akhera.
Al-Zalzalah 99:8
Na yoyote mwenye kufanya baya hata kama ni kwa uzito wa Mdudu Chungu atayaona malipo yake Akhera.
Al-'Adiyat 100:1
Allah Mtukufu Anaapa kwa farasi wenye kwenda Mbio katika njia Yake kumkabili adui, wakitoa sauti kwa kasi ya kukimbia. Haifai kwa kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Allah Mtukufu. Kuapa kwa asiyekuwa Allah Mtukufu ni ushirikina.
Al-'Adiyat 100:2
Na wenye kutoa cheche za moto kwa kwato zao ngumu wanapokimbia kwa kasi.
Al-'Adiyat 100:3
Wenye kushambulia maadui kipindi cha asubuhi.
Al-'Adiyat 100:4
Wakarusha vumbi kwa mbio zao.
Al-'Adiyat 100:5
Wakauweka kati, kwa kuuzunguka kwa vipando vyao, mkusanyiko wa maadui.
Al-'Adiyat 100:6
Hakika binadamu ni mkanushaji sana wa neema za Mola wake.
Al-'Adiyat 100:7
Na yeye anakubali ukanushaji wake.
Al-'Adiyat 100:8
Na yeye ana pupa sana ya kupata mali na anaipenda sana.
Al-'Adiyat 100:9
Kwani binadamu hajui linalomngojea mbele yake, pindi Allah Mtukufu Atakapowatoa wafu makaburini waende kuhesabiwa na kulipwa?
Al-'Adiyat 100:10
Na yakatolewa yaliyo ndani ya vifua: mema na maovu?.
Al-'Adiyat 100:11
Hakika Mola wao siku hiyo ni mwenye kuwatambua wao na mali zao hakuna chenye kufichika Kwake.
Al-Qari'ah 101:1
Kiyama chenye kugonga nyoyo za watu kwa vitisho vyake.
Al-Qari'ah 101:2
Ni kitu gani hicho chenye kugonga?
Al-Qari'ah 101:3
Na ni kipi kilichokujulisha ni kipi hicho chenye kugonga?
Al-Qari'ah 101:4
Siku hiyo watu watakuwa, kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama panzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni.
Al-Qari'ah 101:5
Na majabali yatakuwa ni kama pamba yenye rangi tofauti inayochambuliwa kwa mkono ikawa kama vumbi jembamba na ikamalizika.
Al-Qari'ah 101:6
Basi mwenye kuwa mizani za mema yake ni nzito, zikashinda mabaya yake.
Al-Qari'ah 101:7
Atakua kwenye maisha ya kuridhika Peponi.
Al-Qari'ah 101:8
Ama mwenye kuwa mizani za mema yake ni nyepesi na mizani za maovu yake ni nzito.
Al-Qari'ah 101:9
Makazi yake yatakuwa ni Moto wa Jahanamu.
Al-Qari'ah 101:10
Ni kipi kilichokujulisha, (ewe Mtume), ni ipi hii Jahanamu inayoitwa «Hāwiyah»?
Al-Qari'ah 101:11
Ni Moto unaowaka sana kutokana na vinavyochomwa ndani yake.
Al-Takathur 102:1
Kumekushughulisheni kujifakharisha na mali na watoto, mkaacha kumtii Allah Mtukufu.
Al-Takathur 102:2
Kujishughulisha kwenu na hilo kumeendelea mpaka mkafariki na mkazikwa makaburini.
Al-Takathur 102:3
Sio sawa hivi mnavyofanya vya kushindana kwa wingi wa mali. kwani itawadhihirikia na mtajua kuwa Nyumba ya Akhera ni bora kwenu.
Al-Takathur 102:4
Kisha eleweni kua mtaujua mwisho mbaya wa kutojishughulisha na Akhera.
Al-Takathur 102:5
Sio sawa hivi mnavyofanya vya kushindana kwa wingi wa mali. Lau mngejua uhakika wa adhabu mtakayoipata mngehangaika ili kuokoa nafsi zenu kutoka kwenye maangamivu.
Al-Takathur 102:6
Mtauona Moto!
Al-Takathur 102:7
Kisha mtauona kwa yakini kabisa na bila shaka yoyote.
Al-Takathur 102:8
Kisha mtaulizwa kuhusu kila aina za neema mlizopewa.
Al-'Asr 103:1
Allah Mtukufu Anaapa kwa zama.
Al-'Asr 103:2
Kwamba hakika wanadamu wako kwenye hasara na maangamivu. Haifai kwa mja kuapa isipokuwa kwa Allah Mtukufu, kwani kuapa kwa asiyekuwa Allah Mtukufu ni ushirikina.
Al-'Asr 103:3
Isipokuwa wale waliomuamini Allah Mtukufu, wakafanya amali njema, wakausiana wao kwa wao kushikamana na haki, kufanya matendo ya kumtii Allah Mtukufu na kusubiri juu yake, wao hawatakua kwenye hasara na maangamivu.
Al-Humazah 104:1
Shari na maangamivu yatampata kila mwenye kusengenya watu na kuwatia doa na kuwatusi.
Al-Humazah 104:2
Ambaye hamu yake ni kukusanya mali na kuihesabu.
Al-Humazah 104:3
Akidhani kuwa mali yake ambayo ameikusanya itampa dhamana ya kuishi milele duniani na kukwepa kuhesabiwa akhera.
Al-Humazah 104:4
Anavyodhania sivyo. Atatiwa ndani ya Moto ambao huvunjavunja kila kinachotiwa humo.
Al-Humazah 104:5
Na nikipi kilichokujulisha (ewe Mtume), kua ni upi huo Moto unaovunjavunja?
Al-Humazah 104:6
Huo ni Moto wa Allah Mtukufu uliowashwa.
Al-Humazah 104:7
Ambao kwa ukali wake hupenyeza miilini na kufika kwenye nyoyo.
Al-Humazah 104:8
Hakika moto huo ni wenye kufungwa na kutiwa minyororo huku watu hao wa motoni wakiwa ndani yake.
Al-Humazah 104:9
Minyororo hiyo ni yenye kufungwa kwenye nguzo ndefu.
Al-Fil 105:1
Je hujui na hukusikia, (ewe Mtume), namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Al ka‘ba tukufu?
Al-Fil 105:2
Kwani hakuifanya mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu?
Al-Fil 105:3
Na Aliwapelekea makundi ya ndege yaliyofuatana.
Al-Fil 105:4
Ndege hao walikua wakiwatupia vijiwe vya udongo mkavu na mgumu.
Al-Fil 105:5
Vijiwe hivyo vikawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na kisha kutupwa.
Quraysh 106:1
Oneni ajabu ya mazowea ya makureishi, na amani walionayo, na kuwaendea uzuri mambo yao.
Quraysh 106:2
Oneni ajabu kwa kupangika na kuwepesika kwa misafara yao ya kwenda yemeni kipindi cha kusi na kwenda Shamu kipindi cha kaskazi, ili kuleta vitu wanavyohitajia, na kuwa yote hayo yamewepesishwa na Allah Mtukufu.
Quraysh 106:3
Basi, wamshukuru na kumuabudu Bwana wa Nyumba hii ya Al Ka‘ba, ambayo kwa ajili Yake wamepewa cheo na ukarimu, na wampwekeshe na kumtakasia ibada mola wa nyumba hiyo ya Al Ka‘ba.
Quraysh 106:4
Mola ambaye Amewapa chakula wakati wa njaa kali, na akawapa amani na utulivu dhidi ya hofu iliyokua kubwa sana.
Al-Ma'un 107:1
Je, umeiona hali ya yule ambaye anakanusha kufufuliwa na kulipwa?
Al-Ma'un 107:2
Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu, akimnyima haki zake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake.
Al-Ma'un 107:3
Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha?
Al-Ma'un 107:4
Basi adhabu kali itawafikia wenye kuswali.
Al-Ma'un 107:5
Nao ni wale ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawaziswali kwa nyakati zake.
Al-Ma'un 107:6
Na ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria.
Al-Ma'un 107:7
Na wanakataa kuwaazima watu vitu ambavyo hawadhuriki kwa kuviazima, kama vyombo vya kutumia, na vinginevyo. Wao hawakujifanyia wema nafsi zao kwa kumuabudu Mola wao, wala hawakuwafanyia wema viumbe Vyake.
Al-Kawthar 108:1
Hakika sisi tumekupa, (ewe Nabii), kheri nyingi za dunia na Akhera, miongoni mwazo ni mto wa Kauthar ulioko Peponi, ambao pembezoni mwake ni mahema ya lulu, na mchanga wake ni miski.
Al-Kawthar 108:2
Basi, mtakasie Mola wako ibada zako zote, na uchinje mnyama wako kwa ajili Yake, Peke Yake, pamoja na kutaja jina Lake.
Al-Kawthar 108:3
Mwenye kukuchukia na kuyachukia uliyokuja nayo ya uongofu na nuru: ndiye itakayokatika athari yake, na yeye mwenyewe atakatikiwa na kila kheri.
Al-Kafirun 109:1
Sema, (ewe Mtume), kuwaambia waliomkufuru Allah Mtukufu na Mtume wake: «Enyi wenye kumkanusha Allah Mtukufu!»
Al-Kafirun 109:2
Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo.
Al-Kafirun 109:3
Wala nyinyi si wenye kuabudu Mola Mmoja ninayemuabudu Ambaye ndiye Anayestahiki kuabudiwa.
Al-Kafirun 109:4
Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo.
Al-Kafirun 109:5
Wala nyinyi si wenye kumuabudu ninayemuabudu mimi siku zijazo, Aya hii imeteremka juu ya watu makhsusi miongoni mwa washirikina ambao Allah Mtukufu Alijua kuwa hawataamini kabisa.
Al-Kafirun 109:6
Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ninayo iamini na sitaki nyingine.
Al-Nasr 110:1
Utakapotimia kwako, (ewe Mtume), ushindi dhidi ya makafiri wa kikureishi na ukaikomboa Makkah.
Al-Nasr 110:2
Na ukaona watu wengi wanaingia kwenye Dini ya Allah Mtukufu makundi kwa makundi.
Al-Nasr 110:3
Yatakapotokea hayo, basi jitayarishe kukutana na Mola Wako kwa kumtakasa na kumhimidi na kumuomba msamaha kwa wingi. Kwani Yeye ni Mwingi wa kuwakubalia toba wenye kumsabihi na kumuomba msamaha, kwa kuwasamehe na kuwarehemu.
Al-Masad 111:1
Imepata hasara mikono miwili ya Abū Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia, kwa kumuudhi Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). na kwa hakika ilitimia na kutokea hasara ya abû lahab.
Al-Masad 111:2
Haikumnufaisha mali yake na watoto wake. Kwani hivyo havitamkinga na adhabu ya Allah Mtukufu.
Al-Masad 111:3
Ataingia kwenye Moto wenye mapande makubwa ya moto yanayochomoza kama ulimi.
Al-Masad 111:4
Atauingia moto huo yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ili kumuudhi.
Al-Masad 111:5
Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini.
Al-Ikhlas 112:1
Sema, (ewe Mtume), «Yeye Ndiye Allah Mtukufu Aliyepwekeka kwa ustahiki wa kuabudiwa, uumbaji na utakatifu wa Majina na sifa zake, Asiye na mshirika katika hayo».
Al-Ikhlas 112:2
Allah Mtukufu Peke Yake Ndiye Mwenye kukusudiwa na viumbe katika kutaka kukidhiwa haja zao.
Al-Ikhlas 112:3
Hana mtoto wala wazazi wala mke.
Al-Ikhlas 112:4
Wala hakuna yoyote katika viumbe Vyake mwenye kufanana wala kushabihiyana naye katika Majina Yake, Sifa Zake na vitendo Vyake.
Al-Falaq 113:1
Sema, (ewe Mtume), «Najilinda na kutaka hifadhi kwa muumbaji wa asubuhi».
Al-Falaq 113:2
Kutokana na shari ya viumbe na maudhi yao.
Al-Falaq 113:3
Na kutokana na shari ya usiku wenye giza kubwa uingiapo na ujikitapo, na kutokana na shari na maudhi mbalimbali yaliyomo ndani yake.
Al-Falaq 113:4
Na kutokana na shari za wchawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga.
Al-Falaq 113:5
Na kutokana na shari za hasidi mwenye kuchukia watu, anapowahusudu na kuwadhuru, kwa kutaka neema za Allah Mtukufu alizowaneemesha ziwaondokee.
Al-Nas 114:1
Sema, (ewe Mtume), «Ninajilinda na kutaka hifadhi kwa mlezi wa watu, Mwenye uwezo, Peke Yake, wa kuzizuia shari za shetani».
Al-Nas 114:2
Mfalme wa watu, Mwenye kuendesha mambo yao yote Anavyotaka, Aliye mkwasi wa kutowahitajia.
Al-Nas 114:3
Mola wa watu, Ambaye hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye.
Al-Nas 114:4
Najilinda kwake kutokana na maudhi ya shetani ambaye huwatia watu wasiwasi pale wanapoghafilika kumtaja Allah, na hujificha pale wanapomtaja Allah Mtukufu.
Al-Nas 114:5
Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu.
Al-Nas 114:6
Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.