Lafzullah

Svahilice Meal — Rowad Tercüme Merkezi — Al-Shams 91:1 – Al-Nas 114:6

Author / source: Rowad Tercüme Merkezi — QuranEnc.com (v1.0.5)

Contents
  1. Al-Shams 91:1
  2. Al-Shams 91:2
  3. Al-Shams 91:3
  4. Al-Shams 91:4
  5. Al-Shams 91:5
  6. Al-Shams 91:6
  7. Al-Shams 91:7
  8. Al-Shams 91:8
  9. Al-Shams 91:9
  10. Al-Shams 91:10
  11. Al-Shams 91:11
  12. Al-Shams 91:12
  13. Al-Shams 91:13
  14. Al-Shams 91:14
  15. Al-Shams 91:15
  16. Al-Layl 92:1
  17. Al-Layl 92:2
  18. Al-Layl 92:3
  19. Al-Layl 92:4
  20. Al-Layl 92:5
  21. Al-Layl 92:6
  22. Al-Layl 92:7
  23. Al-Layl 92:8
  24. Al-Layl 92:9
  25. Al-Layl 92:10
  26. Al-Layl 92:11
  27. Al-Layl 92:12
  28. Al-Layl 92:13
  29. Al-Layl 92:14
  30. Al-Layl 92:15
  31. Al-Layl 92:16
  32. Al-Layl 92:17
  33. Al-Layl 92:18
  34. Al-Layl 92:19
  35. Al-Layl 92:20
  36. Al-Layl 92:21
  37. Al-Duha 93:1
  38. Al-Duha 93:2
  39. Al-Duha 93:3
  40. Al-Duha 93:4
  41. Al-Duha 93:5
  42. Al-Duha 93:6
  43. Al-Duha 93:7
  44. Al-Duha 93:8
  45. Al-Duha 93:9
  46. Al-Duha 93:10
  47. Al-Duha 93:11
  48. Al-Sharh 94:1
  49. Al-Sharh 94:2
  50. Al-Sharh 94:3
  51. Al-Sharh 94:4
  52. Al-Sharh 94:5
  53. Al-Sharh 94:6
  54. Al-Sharh 94:7
  55. Al-Sharh 94:8
  56. Al-Tin 95:1
  57. Al-Tin 95:2
  58. Al-Tin 95:3
  59. Al-Tin 95:4
  60. Al-Tin 95:5
  61. Al-Tin 95:6
  62. Al-Tin 95:7
  63. Al-Tin 95:8
  64. Al-'Alaq 96:1
  65. Al-'Alaq 96:2
  66. Al-'Alaq 96:3
  67. Al-'Alaq 96:4
  68. Al-'Alaq 96:5
  69. Al-'Alaq 96:6
  70. Al-'Alaq 96:7
  71. Al-'Alaq 96:8
  72. Al-'Alaq 96:9
  73. Al-'Alaq 96:10
  74. Al-'Alaq 96:11
  75. Al-'Alaq 96:12
  76. Al-'Alaq 96:13
  77. Al-'Alaq 96:14
  78. Al-'Alaq 96:15
  79. Al-'Alaq 96:16
  80. Al-'Alaq 96:17
  81. Al-'Alaq 96:18
  82. Al-'Alaq 96:19
  83. Al-Qadr 97:1
  84. Al-Qadr 97:2
  85. Al-Qadr 97:3
  86. Al-Qadr 97:4
  87. Al-Qadr 97:5
  88. Al-Bayyinah 98:1
  89. Al-Bayyinah 98:2
  90. Al-Bayyinah 98:3
  91. Al-Bayyinah 98:4
  92. Al-Bayyinah 98:5
  93. Al-Bayyinah 98:6
  94. Al-Bayyinah 98:7
  95. Al-Bayyinah 98:8
  96. Al-Zalzalah 99:1
  97. Al-Zalzalah 99:2
  98. Al-Zalzalah 99:3
  99. Al-Zalzalah 99:4
  100. Al-Zalzalah 99:5
  101. Al-Zalzalah 99:6
  102. Al-Zalzalah 99:7
  103. Al-Zalzalah 99:8
  104. Al-'Adiyat 100:1
  105. Al-'Adiyat 100:2
  106. Al-'Adiyat 100:3
  107. Al-'Adiyat 100:4
  108. Al-'Adiyat 100:5
  109. Al-'Adiyat 100:6
  110. Al-'Adiyat 100:7
  111. Al-'Adiyat 100:8
  112. Al-'Adiyat 100:9
  113. Al-'Adiyat 100:10
  114. Al-'Adiyat 100:11
  115. Al-Qari'ah 101:1
  116. Al-Qari'ah 101:2
  117. Al-Qari'ah 101:3
  118. Al-Qari'ah 101:4
  119. Al-Qari'ah 101:5
  120. Al-Qari'ah 101:6
  121. Al-Qari'ah 101:7
  122. Al-Qari'ah 101:8
  123. Al-Qari'ah 101:9
  124. Al-Qari'ah 101:10
  125. Al-Qari'ah 101:11
  126. Al-Takathur 102:1
  127. Al-Takathur 102:2
  128. Al-Takathur 102:3
  129. Al-Takathur 102:4
  130. Al-Takathur 102:5
  131. Al-Takathur 102:6
  132. Al-Takathur 102:7
  133. Al-Takathur 102:8
  134. Al-'Asr 103:1
  135. Al-'Asr 103:2
  136. Al-'Asr 103:3
  137. Al-Humazah 104:1
  138. Al-Humazah 104:2
  139. Al-Humazah 104:3
  140. Al-Humazah 104:4
  141. Al-Humazah 104:5
  142. Al-Humazah 104:6
  143. Al-Humazah 104:7
  144. Al-Humazah 104:8
  145. Al-Humazah 104:9
  146. Al-Fil 105:1
  147. Al-Fil 105:2
  148. Al-Fil 105:3
  149. Al-Fil 105:4
  150. Al-Fil 105:5
  151. Quraysh 106:1
  152. Quraysh 106:2
  153. Quraysh 106:3
  154. Quraysh 106:4
  155. Al-Ma'un 107:1
  156. Al-Ma'un 107:2
  157. Al-Ma'un 107:3
  158. Al-Ma'un 107:4
  159. Al-Ma'un 107:5
  160. Al-Ma'un 107:6
  161. Al-Ma'un 107:7
  162. Al-Kawthar 108:1
  163. Al-Kawthar 108:2
  164. Al-Kawthar 108:3
  165. Al-Kafirun 109:1
  166. Al-Kafirun 109:2
  167. Al-Kafirun 109:3
  168. Al-Kafirun 109:4
  169. Al-Kafirun 109:5
  170. Al-Kafirun 109:6
  171. Al-Nasr 110:1
  172. Al-Nasr 110:2
  173. Al-Nasr 110:3
  174. Al-Masad 111:1
  175. Al-Masad 111:2
  176. Al-Masad 111:3
  177. Al-Masad 111:4
  178. Al-Masad 111:5
  179. Al-Ikhlas 112:1
  180. Al-Ikhlas 112:2
  181. Al-Ikhlas 112:3
  182. Al-Ikhlas 112:4
  183. Al-Falaq 113:1
  184. Al-Falaq 113:2
  185. Al-Falaq 113:3
  186. Al-Falaq 113:4
  187. Al-Falaq 113:5
  188. Al-Nas 114:1
  189. Al-Nas 114:2
  190. Al-Nas 114:3
  191. Al-Nas 114:4
  192. Al-Nas 114:5
  193. Al-Nas 114:6

Al-Shams 91:1

Ninaapa kwa jua na mwangaza wake!

Al-Shams 91:2

Na kwa mwezi unapolifuatia!

Al-Shams 91:3

Na kwa mchana unapolidhihirisha!

Al-Shams 91:4

Na kwa usiku unapolifunika!

Al-Shams 91:5

Na kwa mbingu na kwa aliyeijenga!

Al-Shams 91:6

Na kwa ardhi na kwa aliyeitandaza!

Al-Shams 91:7

Na kwa nafsi na kwa aliyeitengeneza!

Al-Shams 91:8

Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake.

Al-Shams 91:9

Hakika amefanikiwa aliyeitakasa.

Al-Shams 91:10

Na hakika amehasiri aliyeiviza.

Al-Shams 91:11

Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotovu wao.

Al-Shams 91:12

Aliposimama mwovu wao mkubwa.

Al-Shams 91:13

Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipowaambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.

Al-Shams 91:14

Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.

Al-Shams 91:15

Wala Yeye haogopi matokeo yake.

Al-Layl 92:1

Ninaapa kwa usiku unapofunika!

Al-Layl 92:2

Na mchana unapodhihiri!

Al-Layl 92:3

Na kwa aliyeumba dume na jike!

Al-Layl 92:4

Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.

Al-Layl 92:5

Ama mwenye kutoa na akamcha Mungu.

Al-Layl 92:6

Na akalisadiki lililo jema.

Al-Layl 92:7

Tutamrahisishia yawe mepesi.

Al-Layl 92:8

Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake.

Al-Layl 92:9

Na akakanusha lililo jema.

Al-Layl 92:10

Tutamrahisishia yawe mazito!

Al-Layl 92:11

Na mali yake itamfaa nini atakapokuwa anadidimia?

Al-Layl 92:12

Hakika ni juu yetu kuonyesha uongofu.

Al-Layl 92:13

Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.

Al-Layl 92:14

Basi nakuonyeni kutokana na Moto unaowaka vikali.

Al-Layl 92:15

Hatauingia ila mwovu kabisa!

Al-Layl 92:16

Anayekadhibisha na akageuka na kwenda zake.

Al-Layl 92:17

Na mcha Mungu ataepushwa nao.

Al-Layl 92:18

Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.

Al-Layl 92:19

Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliyemfanyia hisani ndiyo anamlipa.

Al-Layl 92:20

Ila ni kutaka uso wa Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.

Al-Layl 92:21

Naye atakujaridhia!

Al-Duha 93:1

Ninaapa kwa wakati wa kabla ya adhuhuri!

Al-Duha 93:2

Na kwa usiku unapotanda!

Al-Duha 93:3

Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.

Al-Duha 93:4

Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko uliotangulia.

Al-Duha 93:5

Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.

Al-Duha 93:6

Kwani hakukukuta yatima, akakupa makazi?

Al-Duha 93:7

Na akakukuta umepotea, akakuongoa?

Al-Duha 93:8

Akakukuta mhitaji akakutosheleza?

Al-Duha 93:9

Basi yatima usimwonee!

Al-Duha 93:10

Na anayeomba au kuuliza usimkaripie!

Al-Duha 93:11

Na neema za Mola wako Mlezi zisimulie.

Al-Sharh 94:1

Hatukukunjulia kifua chako?

Al-Sharh 94:2

Na tukakuondolea mzigo wako.

Al-Sharh 94:3

Uliovunja mgongo wako?

Al-Sharh 94:4

Na tukakunyanyulia utajo wako?

Al-Sharh 94:5

Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi.

Al-Sharh 94:6

Hakika pamoja na uzito upo wepesi.

Al-Sharh 94:7

Na ukipata faragha, fanya juhudi.

Al-Sharh 94:8

Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.

Al-Tin 95:1

Ninaapa kwa tini na zaituni!

Al-Tin 95:2

Na kwa Mlima wa Sinai!

Al-Tin 95:3

Na kwa Mji huu wenye amani mno!

Al-Tin 95:4

Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.

Al-Tin 95:5

Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!

Al-Tin 95:6

Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema, hao watapata ujira usiokwisha.

Al-Tin 95:7

Basi ni kipi baadaye kitakachokukukadhibishia malipo?

Al-Tin 95:8

Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu zaidi kuliko wote wanaohukumu?

Al-'Alaq 96:1

Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba.

Al-'Alaq 96:2

Amemuumba binaadamu kwa tone la damu.

Al-'Alaq 96:3

Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!

Al-'Alaq 96:4

Ambaye amefundisha kwa kalamu.

Al-'Alaq 96:5

Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui.

Al-'Alaq 96:6

Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri.

Al-'Alaq 96:7

Akijiona katajirika.

Al-'Alaq 96:8

Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.

Al-'Alaq 96:9

Umemuona yule anayemkataza.

Al-'Alaq 96:10

Mja anaposali?

Al-'Alaq 96:11

Umeona kama yeye yuko juu ya uongofu?

Al-'Alaq 96:12

Au anaamrisha ucha Mungu?

Al-'Alaq 96:13

Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?

Al-'Alaq 96:14

Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?

Al-'Alaq 96:15

Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!

Al-'Alaq 96:16

Shungi la uongo, lenye makosa!

Al-'Alaq 96:17

Basi na awaite wenzake!

Al-'Alaq 96:18

Nasi tutawaita Mazabania!

Al-'Alaq 96:19

Hasha! Usimtii! Nawe sujudu na ujongee!

Al-Qadr 97:1

Hakika Sisi tumeiteremsha Qur-ani katika Laylatul Qadri (Usiku wa Cheo Kitukufu).

Al-Qadr 97:2

Na nini kitachokujulisha nini Laylatul Qadri?

Al-Qadr 97:3

Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.

Al-Qadr 97:4

Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.

Al-Qadr 97:5

Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.

Al-Bayyinah 98:1

Hawakuwa waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache waliyo nayo mpaka iwajie bayana.

Al-Bayyinah 98:2

Yaani Mtume aliyetoka kwa Mwenyezi Mungu anayewasomea kurasa zilizotakasika.

Al-Bayyinah 98:3

Ndani yake mna maandiko yaliyonyooka.

Al-Bayyinah 98:4

Wala hawakufarikiana waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia hiyo bayana.

Al-Bayyinah 98:5

Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.

Al-Bayyinah 98:6

Hakika waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa.

Al-Bayyinah 98:7

Hakika walioamini na wakatenda mema, hao ndio bora wa viumbe.

Al-Bayyinah 98:8

Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za mbinguni za daima, zipitazo mito kati yake. Wakae humo milele. Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao wa radhi naye. Hayo ni kwa anayemwogopa Mola wake Mlezi.

Al-Zalzalah 99:1

Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!

Al-Zalzalah 99:2

Na itakapotoa ardhi mizigo yake!

Al-Zalzalah 99:3

Na mtu akasema: "Ina nini?"

Al-Zalzalah 99:4

Siku hiyo itahadithia habari zake.

Al-Zalzalah 99:5

Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!

Al-Zalzalah 99:6

Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!

Al-Zalzalah 99:7

Basi anayetenda chembe ya wema, atauona!

Al-Zalzalah 99:8

Na anayetenda chembe ya uovu, atauona!

Al-'Adiyat 100:1

Ninaapa kwa farasi waendao mbio wakipumua.

Al-'Adiyat 100:2

Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini.

Al-'Adiyat 100:3

Wakishambulia wakati wa asubuhi.

Al-'Adiyat 100:4

Huku wakitimua vumbi.

Al-'Adiyat 100:5

Na wakijitoma kati ya kundi.

Al-'Adiyat 100:6

Hakika mwanadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!

Al-'Adiyat 100:7

Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!

Al-'Adiyat 100:8

Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!

Al-'Adiyat 100:9

Kwani hajui watakapofufuliwa waliomo makaburini?

Al-'Adiyat 100:10

Na yakakusanywa yaliyomo vifuani?

Al-'Adiyat 100:11

Hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na habari zao wote!

Al-Qari'ah 101:1

Inayogonga!

Al-Qari'ah 101:2

Ni nini inayogonga?

Al-Qari'ah 101:3

Na ni nini kitachokujulisha ni nini inayogonga?

Al-Qari'ah 101:4

Siku ambayo watu watakuwa kama nondo waliotawanywa;

Al-Qari'ah 101:5

Na milima itakuwa kama sufu zilizochambuliwa!

Al-Qari'ah 101:6

Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito.

Al-Qari'ah 101:7

Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.

Al-Qari'ah 101:8

Na yule ambaye mizani zake zitakuwa hafifu.

Al-Qari'ah 101:9

Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!

Al-Qari'ah 101:10

Na ni nini kitachokujulisha ni nini hiyo?

Al-Qari'ah 101:11

Ni Moto mkali!

Al-Takathur 102:1

Kumekushughulisheni kutafuta wingi.

Al-Takathur 102:2

Mpaka mkaja makaburini!

Al-Takathur 102:3

Sivyo hivyo! Mtakujajua!

Al-Takathur 102:4

Tena sivyo hivyo! Mtakujajua!

Al-Takathur 102:5

Sivyo hivyo! Lau mngelijua kwa elimu ya yakini.

Al-Takathur 102:6

Basi bila ya shaka mtaiona Jahiimu!

Al-Takathur 102:7

Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.

Al-Takathur 102:8

Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema zote.

Al-'Asr 103:1

Ninaapa kwa Zama!

Al-'Asr 103:2

Hakika binadamu bila ya shaka yuko katika hasara.

Al-'Asr 103:3

Ila wale walioamini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri.

Al-Humazah 104:1

Ole wake kila anayewakejeli watu kwa ishara na maneno.

Al-Humazah 104:2

Aliyekusanya mali na kuihesabu.

Al-Humazah 104:3

Anadhani ya kuwa mali yake itambakisha milele!

Al-Humazah 104:4

Hasha! Hakika atavurumishwa katika Hutwama.

Al-Humazah 104:5

Na ni nini kitakachokujulisha ni nini Hutwama?

Al-Humazah 104:6

Ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa.

Al-Humazah 104:7

Ambao unapanda nyoyoni.

Al-Humazah 104:8

Hakika huo utafungwa sawasawa nao wako ndani yake.

Al-Humazah 104:9

Kwenye nguzo zilizonyooshwa.

Al-Fil 105:1

Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyowafanya wale wenye tembo?

Al-Fil 105:2

Kwani hakufanya vitimbi vyao kuharibika?

Al-Fil 105:3

Na akawatumia ndege makundi kwa makundi.

Al-Fil 105:4

Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni.

Al-Fil 105:5

Akawafanya kama majani yaliyoliwa!

Quraysh 106:1

Kwa walivyozoea Maqureshi.

Quraysh 106:2

Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto.

Quraysh 106:3

Basi na wamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii.

Quraysh 106:4

Ambaye anawalisha kutokana na njaa, na anawalinda kutokana na hofu.

Al-Ma'un 107:1

Je, umemwona anayekadhibisha Malipo?

Al-Ma'un 107:2

Basi huyo ndiye anayemsukuma yatima.

Al-Ma'un 107:3

Wala hahimizi kumlisha masikini.

Al-Ma'un 107:4

Basi, ole wao wanaoswali.

Al-Ma'un 107:5

Ambao wanapuuza Swala zao.

Al-Ma'un 107:6

Ambao wanajionyesha.

Al-Ma'un 107:7

Na wanazuia msaada.

Al-Kawthar 108:1

Hakika tumekupa Al-Kawthar (heri nyingi).

Al-Kawthar 108:2

Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.

Al-Kawthar 108:3

Hakika anayekuchukia ndiye aliye mpungufu mno.

Al-Kafirun 109:1

Sema: Enyi makafiri!

Al-Kafirun 109:2

Siabudu mnachokiabudu;

Al-Kafirun 109:3

Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu.

Al-Kafirun 109:4

Wala sitaabudu mnachoabudu.

Al-Kafirun 109:5

Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu.

Al-Kafirun 109:6

Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.

Al-Nasr 110:1

Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi.

Al-Nasr 110:2

Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi.

Al-Nasr 110:3

Basi zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha. Hakika Yeye ndiye anayepokea toba mno.

Al-Masad 111:1

Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.

Al-Masad 111:2

Haitamfaa mali yake, wala alivyovichuma.

Al-Masad 111:3

Atauingia Moto wenye mwako mkali.

Al-Masad 111:4

Na mkewe, mchukuzi mkubwa wa kuni.

Al-Masad 111:5

Shingoni mwake iko kamba iliyosokotwa sawasawa.

Al-Ikhlas 112:1

Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa Pekee.

Al-Ikhlas 112:2

Mwenyezi Mungu ndiye Mkusudiwa.

Al-Ikhlas 112:3

Hakuzaa wala hakuzaliwa.

Al-Ikhlas 112:4

Wala hana anayelingana naye hata mmoja.

Al-Falaq 113:1

Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko.

Al-Falaq 113:2

Kutokana na uovu wa alivyoviumba.

Al-Falaq 113:3

Na kutokana na uovu wa giza la usiku liingiapo.

Al-Falaq 113:4

Na kutokana na uovu wa wanaopuliza mafundoni.

Al-Falaq 113:5

Na kutokana na uovu wa mwenye husuda anapohusudu.

Al-Nas 114:1

Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa watu.

Al-Nas 114:2

Mfalme wa watu.

Al-Nas 114:3

Mungu wa watu.

Al-Nas 114:4

Kutokana na uovu wa Shetani mtia wasiwasi, ajifichaye mno (Al-Khannaas).

Al-Nas 114:5

Anayetia wasiwasi katika vifua vya watu.

Al-Nas 114:6

Kutokana na majini na watu.